Rais Donald Trump amesema anasimamisha operesheni ya kijeshi ya Marekani ya kusindikiza meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz "Project Freedom." Uamuzi wa Trump unakuja siku moja baada ya operesheni hiyo kuanza.
Rais Donald Trump amesema
anasimamisha operesheni ya kijeshi ya Marekani ya kusindikiza meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz "Project
Freedom" baada ya siku moja tu, katika juhudi za kufikia makubaliano na
Iran ili kukomesha vita vya Mashariki ya Kati.
Kauli ya Trump imefuatia tangazo la waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio kusema
Jumanne kwamba Marekani imekamilisha shughuli zake za mashambulizi dhidi ya
Iran, ingawa Washington ilionya kuwa iko tayari kujibu vibaya mashambulizi
yoyote mapya dhidi ya meli katika Mlango Bahari wa Hormuz.
Matamshi ya Rubio yalikuja baada ya afisa mkuu wa jeshi la
Marekani kusema vikosi vya Marekani viko tayari kuendelea na shughuli za
mapigano iwapo vitaamriwa.
Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi la Iran lilionya
kuhusu mwitikio thabiti ikiwa meli zitapotoka kutoka kwa njia yake
iliyoidhinishwa kupitia mlango bahari wa Hormuz.
Hata hivyo umoja wa Falme za Kiarabu imesema inazuia mfululizo wa mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran kwa siku ya pili, madai ambayo Iran kimsingi imeyakanusha.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime