OUSMANE DEMBÉLÉ ATWAA TUZO YA UNFP KWA MARA YA PILI MFULULIZO

Nyota wa Paris Saint-Germain, Ousmane Dembélé, ametawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligue 1 (UNFP Player of the Year) kwa msimu wa pili mfululizo (2024/25 na 2025/26).

Licha ya changamoto za majeraha msimu huu, ‘Dembouz’ ameonesha kwanini yeye ni mshindi wa Ballon d’Or 2025 kwa kuiongoza PSG kutawala soka la nyumbani na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika kinyang’anyiro cha msimu huu wa 2025/26, Dembélé alichuana na mastaa watano ambao ni:

Vitinha (Kiungo fundi wa PSG)

Nuno Mendes (Beki wa pembeni mwenye kasi wa PSG)

Florian Thauvin (Mkongwe aliyegeuka lulu huko Lens)

Mason Greenwood (Mshambuliaji hatari wa Marseille)

Dembélé anakuwa mchezaji wa tano katika historia ya ligi hiyo kushinda tuzo hii mara mbili mfululizo, akifuata nyayo za wakongwe kama Zlatan Ibrahimovic.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii