Marie-Louise Eta amekuwa kocha wa kwanza wa kike kushinda mechi katika mojawapo ya ligi tano kuu za kandanda Ulaya.
Hii ni baada ya timu yake ya Union Berlin kuilaza Mainz 3-1katika mechi ya Ligi Kuu ya Kandanda ya Ujerumani, Bundesliga hapo Jumapili.
Baada ya mechi Eta alijumuika na wachezaji wa timu hiyo kwa kusherehekea ushindi huo wa timu yake uliokuja katika mechi yake ya nne kama kocha wa muda.
Huu ndio ulikuwa ushindi wa kwnaza wa Union tangumwezi Machi.
Eta alichukua uongozi wa klabu hiyo baada ya kuachishwa kazi kwa Steffen Baumgart mwezi Aprili.
Hatamu ya Eta kama kocha wa timu ya wanaume ya Union itakwisha mwishoni mwa wiki ijayo hiyo timu yake itakapopambana na Augsburg katika mechi ya mwisho ya msimu.