Mabingwa watetezi VfB Stuttgart, wamefika fainali ya Kombe la Shirikisho la Ujerumani – DFB Pokal kwa mara nyingine tena kutokana na ushindi wa 2-1 baada ya muda wa ziada dhidi ya SC Freiburg Jumatano jioni.
Tiago Tomas alifunga bao la ushindi ambalo lilikuwa maridadi kabisa kwa njia ya kisigino katika dakika za mwisho za muda wa ziada huku mashabiki wa nyumbani wakishangilia kwa furaha.
Freiburg walikuwa wameongoza kupitia kwa Maximilian Eggestein
katika dakika ya 28 lakini Deniz Undav akawasawazishia wenyeji katika dakika ya
70.
"Bila shaka nimefurahi sana, ni ajabu kwamba ushindi huu ulipatikana baada ya dakika 119. Hongera kwanza kwa Freiburg.
Lakini lazima
niipongeze timu yangu, ulikuwa mchezo mgumu kwetu," kocha wa Stuttgart
Sebastian Hoeness aliiambia televisheni ya ARD. "Ninafurahi sana kwamba
haikuenda kwenye mikwaju ya penalti. Nilikuwa na tumbo joto"
Stuttgart sasa watapata nafasi ya kutetea taji lao dhidi ya
mabingwa wa kihistoria Bayern Munich mnamo Mei 23 huko Berlin. Bayern iliishinda Bayer Leverkusen 2-0 Jumanne.
Kipa wa Freiburg Florian Müller aliokoa mashambulizi kadhaa.
"Nimevunjika moyo sana. Tulipambana hadi mwisho. Jinsi
ilivyotokea ni uchungu sana. Inauma sana. Tulipata nafasi kubwa wakati
tulipokuwa kifua mbele 1-0," Müller aliyevunjika moyo aliiambia ARD.
Eggestein aliongeza: "Uungaji mkono kutoka kwa mashabiki ulikuwa mzuri, kushindwa huku kunauma. Inasikitisha sana. Daima kuna mambo ambayo unaweza kuyakosoa, lakini timu zote mbili zilijitolea kwa nguvu zao zote."
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime