Ripoti mpya za kijasusi za Marekani zinaeleza kuwa China inadaiwa kujiandaa kupeleka mifumo mipya ya ulinzi wa anga kwa Iran katika wiki zijazo, wakati ambapo mapigano kati ya Iran na Marekani yamesitishwa kwa muda.
Kwa mujibu wa vyanzo vitatu vilivyozungumza na CNN, vifaa hivyo vinajumuisha mifumo ya makombora ya kubebeka begani (MANPADS), ambayo inaweza kutumika kushambulia ndege zinazoruka chini.
Hatua hiyo inatajwa kuwa inaweza kuongeza mvutano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani, hasa ikizingatiwa kuwa Beijing ilidai kuhusika katika kusaidia kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano hivi karibuni.
Aidha, taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya usafirishaji huo unaweza kupitishwa kupitia nchi za tatu ili kuficha chanzo chake halisi.
Ubalozi wa China nchini Marekani umekanusha madai hayo, ukisema kuwa Beijing haijawahi kuiuzia silaha yoyote pande zinazohusika na mgogoro huo.
“China haijawahi kutoa silaha kwa upande wowote katika mzozo huu,” ilisema taarifa hiyo, ikisisitiza kuwa nchi hiyo inaheshimu sheria za kimataifa na inahimiza amani.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime