Djibouti kufanya uchaguzi wa rais siku ya Ijumaa

Uchaguzi wa rais unafanyika siku ya Ijumaa kwenye taifa hilo lenye umuhimu mkubwa wa kimkakati katika Pembe ya Afrika rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh anatafuta nafasi ya kuiongoza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika  kwa muhula wa sita na atachuana na mgombea mmoja tu asiye na umaarufu sana Mohamed Farah Samatar, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Unified Democratic Center (CDU), ambacho hakina hatakiti kimoja bungeni.

Hata hivyo zaidi ya wapiga kura 256,000 wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo na itakumbukwa kuwa Guelleh ameiongoza nchi hiyo yenye takriban wakaazi milioni moja kwa mkono wa chuma kwa miaka 27. Nchi hiyo ndogo inahifadhi kambi na vikosi vya kijeshi kutoka Ufaransa, Marekani, China, Japan na Italia, jambo linalozalisha faida kubwa za kifedha, kiusalama na kisiasa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii