Mudathir afungiwa Mechi tatu na kutozwa faini

Kiungo wa YangaMudathir Yahya amefungiwa michezo mitatu pamoja na kutozwa faini ya Tsh milioni 1 baada ya kukutwa na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji FCIbrahim Abraham wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kikao kilichofanyika siku ya Aprili 18, 2026, ambapo walipitia matukio mbalimbali ya ligi, likiwemo tukio hilo lililotokea katika uwanja wa CCM Kirumba Stadium. Katika mchezo huo, Young Africans SC waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Kwa mujibu wa ratiba ya adhabu hiyo, Mudathir Yahya atakosa michezo mitatu ya ligi dhidi ya:

  • Simba SC (Mei 3, 2026 – ugenini)
  • KMC FC (Mei 6, 2026 – nyumbani)
  • Coastal Union FC (Mei 9, 2026 – nyumbani)

TPLB imesisitiza kuwa adhabu hizo zinalenga kudhibiti nidhamu uwanjani na kuhakikisha mchezo unachezwa kwa heshima na kuzingatia sheria za soka.

 

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii