Urusi yashambulia bandari ya Odesa nchini Ukraine

Urusi imefanya uharibifu wa meli inayopeperusha bendera ya Panama, iliyokuwa katika bandari ya Odesa nchini Ukraine

Droni za Urusi zimeshambulia bandari ya Izmail kusini mwa mkoa wa Odesa usiku wa kuamkia leo na kusababisha kuiharibu meli ya kiraia iliyokuwa na bendera ya Panama.

Hayo yameelezwa leo na naibu waziri mkuu wa Ukraine Oleksiy Kuleba ambaye ameongeza kusema kwamba uharibifu umefanyika pia dhidi ya miundo mbinu  na vifaa kadhaa kufuatia mashambulio ya Urusi. Kuleba amesema kwa mara nyingine Urusi, ambayo ni adui wa Ukraine, amelenga kwa makusudi miundo mbinu muhimu na vifaa vya usafiri katika mkoa wa Odesa.

Zelensky awasili Berlin kwa mazungumzo na Kansela Merz


Mashambulizi hayo ya Urusi dhidi ya Ukraine yameripotiwa katika wakati ambapo Rais Volodymyr Zelensky akitarajiwa baadae leo mjini Berlin ambako atafanya mazungumzo na Kansela Friedrich Merz kuhusu suala la ufadhili wa kifedha na msaada wa kijeshi na juhudi za ujenzi mpya wa nchi yake.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii