Mahakama moja nchini Senegal imetoa hukumu ya kwanza chini ya sheria mpya iliyoongeza adhabu kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ambayo makundi ya kutetea haki za binadamu yameitaja kuwa ya ukandamizaji.
Kwenye hukumu hiyo mwanaume
mwenye umri wa miaka 24 ametupwa jela kwa miaka sita pamoja na kutozwa faidi ya
faranga milioni 2 sawa na dola 3,300 za Marekani kwa kushiriki vitendo vya ushoga.
Kijana huyo alikamatwa mapema mwezi huu baada ya kupitishwa
sheria iliyoongeza muda wa kifungo jela kuwa kati ya miaka mitano hadi 10 kwa
wanaotiwa hatiani kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Hata hivyo itakumbukwa kuwa Senegal ambalo ni taifa la Afrika Magharibi lenye idadi kubwa ya waislamu, limechukua msimamo mkali dhidi ya vitendo vya ushoga ikizelenga pia asasi inazozituhumu kuunga mkono haki za makundi hayo ya wachache.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime