Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan, Mheshimiwa Anderson Mutatembwa, alipokea kwa niaba ya Serikali msaada wa magari matatu ya zimamoto na uokoaji yaliyotolewa na Taasisi ya Zimamoto ya Japan (Japan Firefighters Association).
Magari hayo ni sehemu ya magari Matano ambayo Taasisi hiyo imepanga kuipatia Tanzania mwaka 2026 na yanatarajiwa kuwasili nchini mwezi Mei 2026.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo wa kutoa magari 30 ndani ya kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2028 ukilenga kuimarisha huduma za zimamoto na uokoaji nchini na kuongeza uwezo wa nchi kukabiliana na majanga.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii