Iran imesema iko kwenye mazungumzo na FIFA kuhusu uwezekano wa kucheza mechi zake za FIFA World Cup nje ya United States kufuatia onyo lililotolewa na Donald Trump.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, mamlaka ya soka ya nchi hiyo inapendekeza mechi zao zifanyike Mexico badala ya Marekani, huku FIFA ikielezwa kuwa bado haijafanya uamuzi wa kubadilisha ratiba ya mashindano hayo.