KLABU ya Simba SC ipo hatua za mwisho kukamilisha makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wake, Kibu Denis, kwenda klabu ya Al Nasr ya Libya.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimethibitisha kuwa nyota huyo tayari anaandaliwa kukamilisha taratibu za mwisho kabla ya kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Al Nasr.
“Kibu anaelekea Libya. Simba na Al Nasr tayari wamekubaliana, kilichobaki ni mambo machache ya kiutawala ili dili lifungwe,” kilieleza chanzo hicho.
Hii si mara ya kwanza kwa Al Nasr kumfuatilia Kibu, kwani ilianza kumhitaji tangu dirisha kubwa la usajili kabla ya msimu huu, lakini safari hiyo haikufanikiwa wakati huo.
Aidha safari hii, Al Nasr wamekuja kwa msimamo tofauti na nguvu ya kifedha, jambo lililoifanya Simba kukubali kumuuza ili kuepuka kumpoteza bure baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo itakumbukwa kuwa mkataba wa Kibu Denis na Simba SC unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo uamuzi wa kumuuza sasa ni mkakati wa klabu kunufaika kifedha kabla nyota huyo hajaondoka bila malipo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime