Simba Yathibitisha Kuondoka kwa Kibu ‘Mkandaji’

Klabu ya Simba SC imethibitisha kwamba mshambuliaji wake, Kibu Dennis, hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo, akihitimisha utumishi wake wa misimu minne na nusu akiwa na Wekundu wa Msimbazi.

Kibu ‘Mkandaji’, ambaye alijiunga na Simba SC miaka kadhaa iliyopita, anaripotiwa kujiunga na klabu ya Al Nasr Benghazi nchini Libya, na kutambulishwa hivi karibuni kama mchezaji mpya wa timu hiyo.

Aidha hatua hii itakuwa mara nyingine kwa Simba SC kuona wachezaji wao wakijiunga na klabu nyingine barani Afrika, huku Kibu akijiunga na Fabrice Ngoma na Steven Desse Mukwala, ambao pia walihama Simba SC kwa nyakati tofauti na kujiunga na Al Nasr Benghazi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii