Raia zaidi ya milioni 21 wa Uganda wanapiga kura Alhamisi ya leo katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kuendeleza utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.
Ikiwa Museveni mwenye umri wa miaka 81 na aliyepo madarakani tangu mwaka 1986 anawania muhula wa saba ambao unatiwa hofu kuhusu uwazi wa mchakato huo hasa wakati huu kukiwa kumezimwa mtandao wa intaneti na mawasiliano.
Aidha Museveni anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine mwenye umri wa miaka 43 anayewakilisha kizazi kinachotamani mabadiliko ya kisiasa katika taifa la Afrika Mashariki lenye watu takribani milioni 45.
Hata hivyo wakati Uganda ikiingia kwenye uchaguzi wa rais hatua za kuzima mtandao kuwepo kwa wanajeshi mitaani na madai ya kuingiliwa kwa mchakato zimeibua maswali mazito kuhusu uwazi wa kura na mustakabali wa demokrasia.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime