Fahamu vinywaji na Vyakula Vinavyosababisha Vidonda vya Tumbo na Jinsi ya Kutibu

Vidonda vya tumbo ( kitaalam Peptic Ulcer) ni majeraha au vidonda vinavyotokea kwenye utando wa ndani wa tumbo au sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum).

Ingawa kuna sababu nyingi za mtu kuwa na vidonda vya tumbo kama ifuatavyo:
Maambukizi ya Bakteria: Sababu kuu ni maambukizi ya bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori). Bakteria hawa huishi kwenye utando wa tumbo na wanaweza kusababisha kuvimba na vidonda.

Matumizi ya Dawa za Maumivu (NSAIDs):

Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu kama vile aspirini na ibuprofen yanaweza kuharibu utando wa tumbo na kusababisha vidonda vya tumbo.

Mambo Mengine: Vyakula vyenye viungo vingi, msongo wa mawazo, na unywaji wa pombe kupita kiasi havisababishi moja kwa moja vidonda, lakini vinaweza kuzidisha dalili za tatizo hilo.

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili za vidonda vya tumbo zinaweza kutofautiana, lakini za kawaida ni pamoja na:
Maumivu makali, yanayowaka, au ya kuuma katikati ya tumbo, hasa wakati tumbo likiwa tupu yaani ukiwa na njaa. Kichefuchefu na kutapika, kupoteza hamu ya kula au kupungua uzito bila sababu.

Dalili nyingine ni kutokwa na damu kwenye kinyesi, ambacho kinaweza kuonekana cheusi na kuhisi tumbo kujaa gesi au kujaa haraka baada ya kula kidogo.

Tiba ya vidonda vya tumbo
Matibabu ya vidonda vya tumbo hutegemea na chanzo chake kama vile:
Dawa: Dawa za kuua bakteria (antibiotics) hutumika kutibu maambukizi ya H. pylori. Pia, dawa zinazopunguza uzalishaji wa asidi ya tumbo, kama vile PPIs (Proton Pump Inhibitors), hutumika kusaidia kuponya vidonda kupona.
Mabadiliko ya Lishe na Maisha: Kuepuka vyakula vinavyochochea dalili, kupunguza matumizi ya pombe, na kuacha kuvuta sigara kunaweza kusaidia katika uponyaji wa vidonda vya tumbo.

Katika hali mbaya, hasa pale kunapotokea kutokwa na damu au kutoboka kwa tumbo, upasuaji unaweza kuhitajika. Ukiona dalili hizo haraka sana kamuone daktari akufanyie vipimo kisha akupe tiba stahiki.

Vyakula vya wenye vidonda vya tumbo
Vyakula ambavyo si rafiki kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na acid refluxni vinywaji vikali kama pombe, soda na juise za viwandani.
-Vinywaji vyenye caffeine kama Kahawa, Maziwa/Cream na products zake.
Pia nyama yenye mafuta mengi, Vyakula vilivyokaangwa (kwa mafuta mengi kama chipsi n.k. Vyakula vyenye viungo vingi, vyakula vyenye chumvi nyingi, vyakula vyenye acid kama vile malimao, ndimu , pilipili nk, Nyanya pamoja na bidhaa zake, Chocolate, vyakula vyenye gesi nyingi kama jamii ya maharage, vyakula vya maganda kama mihogo, ndizi n.k.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii