Ubongo wa mwanadamu ni kiungo muhimu kinachohitaji usambazaji endelevu wa damu ili kupata oksijeni na glukosi kutokana na mtatizo wowote unaokatiza mtiririko wa damu unaweza kusababisha kifo cha seli za ubongo ndani ya dakika chache na kuleta madhara ya kudumu.
Kiharusi cha ubongo ni nini ? (cerebrovascular stroke) ni hali ya dharura ya kiafya inayotokea pale usambazaji wa damu kwenye sehemu ya ubongo unapopungua au kukatika kabisa. Kukosa oksijeni na virutubishi husababisha seli za ubongo kufa, na kwa kuwa haziwezi kuzaliwa upya, madhara yake huwa ya kudumu.
Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata kiharusi ikilinganishwa na wanaume, ingawa dalili nyingi zinafanana kwa wote. Dalili za kawaida ni pamoja na:
Kupooza au kufa ganzi ghafla upande mmoja wa mwili
Uso au midomo kuinamia upande mmoja
Kizunguzungu au kupoteza usawa
Ugumu wa kuongea au kuchanganyikiwa
Kuona kwa shida au kuona kwa jicho moja
Maumivu makali ya ghafla ya kichwa
Ugumu wa kutembea
Kutapika au kupoteza fahamu
Kiharusi hugawanywa katika aina kuu tatu:
Ni aina ya kawaida zaidi, husababishwa na kuziba kwa mshipa wa damu. Hugawanyika katika:
Kiharusi cha Thrombotic: Kuganda kwa damu kutokana na mafuta (plaque) kwenye mishipa ya damu ya ubongo.
Kiharusi cha Embolic: Gando la damu au hewa kutoka sehemu nyingine ya mwili husafiri hadi kwenye ubongo.
Hii ni aina ya kiharusi kidogo ambapo mtiririko wa damu hukatika kwa muda mfupi. Ni onyo kubwa la hatari ya kupata kiharusi kikubwa baadaye.
Sababu nyingi za kiharusi zinahusiana na mtindo wa maisha, zikiwemo:
Maisha ya kukaa bila mazoezi na msongo wa mawazo
Unywaji wa pombe kupita kiasi
Matumizi ya dawa za kulevya kama kokeni
Shinikizo la damu lisilodhibitiwa
Kisukari na kiwango kikubwa cha cholesterol
Uvutaji sigara na matumizi ya tumbaku
Matatizo ya usingizi kama apnea
Magonjwa ya moyo
Aidha Matibabu ya kiharusi hutegemea aina ya kiharusi kilichotokea, huku lengo kuu likiwa kurejesha mtiririko wa damu kwenye ubongo haraka iwezekanavyo. Daktari anaweza kushauri dawa za kuzuia kiharusi kwa watu walio katika hatari kubwa.
Hata hivyo kiharusi cha ubongo ni dharura ya kimatibabu inayohitaji hatua za haraka. Dalili zozote zinapojitokeza, ni muhimu kuwahi hospitali mara moja ili kuokoa maisha na kupunguza madhara ya kudumu.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime