Rais wa Marekani Donald Trump amesema vikosi vya Marekani vimefanya mashambulizi makali dhidi ya kundi linalojiita dola la kiislam IS kaskazini magharibi mwa Nigeria ambapo ametishia kwamba watafanya mashambulizi zaidi.
Aidha Trump amesema kuwa vikosi vya Marekani vimefanya mashambulizi makali dhidi ya kundi linalojiita dola la kiislam IS kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Akiutumia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump amevipongeza vikosi vya Marekani kwa mashambulizi hayo na kuapa kwamba wataendelea kufanya hivyo ikiwa kundi hilo litaendelea kuwaua Wakristo.
Hivyo kamandi ya Marekani barani Afrika imesema mashambulizi hayo iliyosema ni kwa ombi la mamlaka ya Nigeria na kwamba yamewaua magaidi wengi.
Hata hivyo Nigeria kupitia wizara yake ya mambo ya nje imethibitisha mashambulizi hayo na kusema kwamba yamelenga maeneo sahihi ya magaidi wa kundi hilo huku tukio hili la hivi punde linakuja wakati hali ya ukosefu wa usalama ikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime