Katika tukio lililozua mshangao mkubwa mwanaume mmoja ambaye utambulisho wake bado haujafahamika amenaswa akitembea juu ya nyaya za umeme katika eneo la Barangay Ilang jijini Davao City nchini Ufilipino asubuhi ya sikukuu ya Krismasi Desemba 25 mwaka huu.
Tukio hilo la hatari lilirekodiwa kwa video na baadhi ya wakazi wa eneo hilo na kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii likionyesha mwanaume huyo akitembea juu ya nyaya hizo bila ulinzi wowote hali iliyozua hofu na maswali mengi kuhusu usalama wake.
Aidha hadi kufikia sasa mamlaka husika bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu mwanaume huyo ikiwemo utambulisho wake hali yake ya kiafya wala sababu zilizomsukuma kufanya kitendo hicho kisicho cha kawaida na chenye hatari kubwa kwa maisha.
Hata hivyo tukio hilo limeibua mjadala mpana miongoni mwa wananchi huku wengi wakitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka ili kuzuia matukio kama hayo ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa au vifo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime