Katika Maisha ya kila siku Maneno kama hekima na akili hutumika kwa pamoja kana kwamba yana maana moja ambapo Watu wengi husema " Yule mtu ana akili nyingi au ana hekima kubwa" .
Hatahivyo ukichunguza kwa undani ,Maneno haya mawili yana maana zinazo karibiana lakini zina tofauti katika uhalisia wake.
Makala hii inaeleza maana ya uhusiano na tofauti kati ya hekima na akili,pamoja na umuhimu wake katika maisha ya binadamu.
Akili ni kipaji cha asili ambacho binadamu huzaliwa nacho.
Niuwezo wa kufikiri ,kuelewa mambo,kukumbuka,na kufanya maamuzi ya haraka.
Akili humwezesha mtu kutatua matatizo kwa kutumia hoja na mantiki.
Mtu mwenye akili niyule anayeweza kuelewa mambo kwa urahisi ,kufanya hesabu ,kupanga mikakati au kubuni mambo mapya.
Kwamfano:Mwanafunzi mwenye akili nyingi hujifunza kwa haraka na kupata matokeo mazuri darasani .
Hivyo basi akili ni chombo cha msingi cha kufikiri ambacho kila mwanadamu anacho kwa kiwango fulani.
Hekima ni uwezo wakutumia akili kwa uangalifu na busara katika kufanya maamuzi au kutoa ushauri.
Tofauti na akili hekima haipatikani kwa kusoma vitabu pekee,hupatikana kupitia uzoefu wa maisha,mafunzo na tafakari ya kina.
Mtu mwenye hekima ni yule anayefanya uamuzi unaozingatia matokeo ya mbele,anayejua wakati wa kusema na wakati wakunyamaza na anayeheshimu maadili ya jamii.
Kwamfano: Mzee mwenye hekima anaweza kutuliza mzozo mkubwa bila kutumia nguvu,bali maneno yake yenye busara.
Akili na hekima ni ndugu wa karibu: Huwezi kuwa na hekima bila kutumia akili,na akili bila hekima inaweza kuleta hasara ,Akili ni kama mbegu lakini hekima ni tunda .
Akili ni maarifa ,hekima ni matumizi ya maarifa hayo kwa manufaa.Hivyo basi,hekima ni kiwango cha juu cha matumizi ya akili.
Akili humwezesha mtukufanikiwa kielimu na kitaaluma, lakini hekima humsaidia kuishi kwa amani na kuhusiana vyema na watu wengine.
Dunia ya sasa inahitaji watu wenye akili za sayansi na hekima ya kibinadamu .
Akili bila hekima inaweza kuharibu,kama ilivyo kwa sayansi isiyoongozwa na maadili.
Kwaujumla akili ni uwezo wa kufikiri ,na hekima ni uwezo wa kutumia fikra hizo kwa manufaa.
Mtu mwenye akili anaweza kuelewa haraka lakini mwenye hekima anajua nini cha kufanya na lini.
Hivyo basi hekima ni ngao ya maisha,wakati akili ni silaha ya maendeleo.
"Akili hufikiri,hekima huelekeza" Mwenye akili hujua njia ,lakini mwenye hekima huchagua ipasavyo".
Katika vitabu vitakatifu Biblia,na Qur'an tukufu hekima imezungumzwa kama ifuatavyo; Methali 4: 7 inasema " Hekima ndiyo jambo la kwanza basi pata hekima na katika zote upatayo pata ufahamu".
Hii inatuonyesha kuwa hekima ni nguzo ya maisha ,muhimu zaidi hata kuliko maarifa ya kawaida.
Yakobo 1:6" Lakini mtu wa kwenu,akipungukiwa na hekima ,na aombe kwa mungu awapaye wote kwa ukarimu ,wala hakemei ,naye atapewa" Hekima ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa wale wanaoomba kwa imani.
Sura Al- Baqarah( 2:269)" Anampa hekima amtakaye na aliyepewa hekima bila shaka amepewa hekima bila shaka amepewa kheri nyingi,wala hawakumbuki ila wenye akili"Hapa Qur'an inaonyesha kwamba hekima ni neema kubwa kutoka kwa mwenyezi Mungu na wenye akili ndio wanaotambua thamani yake.
Sura Luqman 31:12): " Nahakika tulimpa Luqman hekima,Mushukuru mwenyezi Mungu na mwenye kushukuru basi anajishukuru mwenyewe ,na mwenye kufuru ,basi hakika mwenyezi Mungu ni mkwasi,msifiwa. Hekima inaambatana na moyo wa shukrani na unyenyekevu mbele ya Mungu.
Nivyema na haki kila jambo tunalo litenda kila kuchapo na yanayoendelea tukatawaliwa na akili na hekima ili ikatusaidia kufika katika nchi ya ahadi.