Yacouba Apewa Siku 45 Tu Yanga

DAKTARI wa viungo wa Yanga, Mtunisia, Youssef Ammar, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne, amepata nafuu na atarejea uwanjani baada ya takribani siku 45.

Yacouba yupo nje ya uwanja tangu Novemba mwaka jana alipoumia goti ambapo tayari amepatiwa matibabu nchini Tunisia.

Akizungumza na Jembe FM Ammar alisema Yacouba ameanza program ya mazoezi ya kukimbia mbio fupi na
ndefu kwa ajili ya kujiweka
sawa, ikiwa ni baada ya kumaliza program ya gym.

Aliongeza kuwa nyota huyo atakuwa fiti na kamili kuanza kuipambania timu hiyo, baada ya mwezi mmoja na nusu ambao ni sawa na siku 45.

“Licha ya Yacouba kupata nafuu pamoja  na kuanza program ya mazoezi ya kukimbia mbio fupi na ndefu, lakini bado anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wangu. “Kwani bado hajapona vizuri, hivyo yupo chini ya uangalizi kwa hofu ya kujitonesha ili asirejee tena katika majeraha hayo ya goti.

“Kutokana na maendeleo yake hivi sasa, upo uwezekano wa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja na nusu,” alisema Ammar.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii