Mkutano Mkuu wa mwaka wa wafanyakazi wote wa Taasisi ya MOI umefanyika leo Oktoba 03 mwaka huu katika ukumbi wa CPL Muhimbili jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi kutoka vitengo mbalimbali vya taasisi hiyo.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema
“Wafanyakazi wenzangu leo tumekusanyika hapa kwa lengo la kujadiliana pamoja namna ya kuboresha huduma katika Taasisi yetu, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili, kuongeza uwajibaki na uadilifu ili kuboresha huduma kwa wagonjwa wetu kwano kila mmoja ana nafasi ya kuchangia mafanikio ya MOI.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Orest Mushi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi ili kufikia malengo ya Taasisisi.
“Mkutano huu ni utekelezaji wa azimio la Kikao cha Baraza kilichopita na unalenga kujenga uelewa na mshirikiano wa kweli. Ni jukwaa la kusikiliza kero, ushauri na maoni ya watumishi ili tuweze kuboresha mazingira ya kazi.”
Mkutano wa watumishi wa MOI umejumuisha wawakilishi kutoka katika kila kitengo na idara lengo ikiwa ni kuleta umoja baina ya wafanyakazi na kuhakikisha Taasisi inazidi kupiga hatua katika kutoa huduma bora kwa wananchi.