Mauzo ya magari yapungua kufuatia ongezeko la ushuru wa Marekani

Madhara ya kwanza ya mashambulizi ya kibiashara ya Marekani yanaonekana nchini Afrika Kusini. Usafirishaji wa magari kwenda Marekani umepungua kwa 73% katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka Sekta ya magari inahofia maisha yake ya baadaye.

"Mgogoro wa kijamii unakuja": haya ni maneno ya Mikel Mabasa, Mkurugenzi Mkuu wa chama cha makampuni ya kutengeneza magari Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa  Julai 15 mwaka huu chama hicho cha makampuni ya kutengeneza magari kimeonyesha wasiwasi wake. Takwimu zote za usafirishaji ziko kwenye mstari mwekundu. Mnamo mwezi Aprili na Mei, mauzo ya magari yaliyotengenezwa nchini Afrika Kusini kwenda Marekani yalipungua kwa 80%.

Marekani ni mshirika wa pili wa kibiashara nchini Afrika Kusini. Mnamo mwaka 2024, sekta ya magari ya Afrika Kusini ilichangia 64% ya biashara zote chini ya makubaliano ya AGOA na Washington, ambayo inaonyesha ni kwa kiasi gani ushuru uliowekwa na Donald Trump unaathiri sekta hiyo.

Tayari kulikuwa na asilimia 25 ya ushuru wa ziada kwa magari mwezi Aprili, na kuanzia tarehe Mosi Agosti, kiwango kipya cha ushuru wa forodha cha 30% kitatumika kwa mauzo yote ya nje ya Afrika Kusini.

Mlolongo mzima wa ugavi huenda ukaathirika. Kutoka kwa watengenezaji wa sehemu hadi watoa huduma wa vifaa, ambao watalazimika kuachisha kazi haraka wafanyakazi. Chrysler, Stellantis, na hata Mercedes Benz… makampuni ya kigeni ya kutengeneza magari yanaweza kuamua kupunguza kwa kiasi kikubwa utendakazi wao nchini Afrika Kusini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii