Uchaguzi wa CWT umetangaza Suleiman Ikomba kuwa rais mpya

Hatimaye  tambo na majigambo ya wagombea wa nafasi ya urais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) zimekwisha baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa chama hicho Suleiman Ikomba kutangazwa mshindi wa kiti cha urais wa chama hicho akimbwaga Mwalimu Leah Ulaya aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.

Wawili hao walikuwa wamevuta hisia za walimu ambapo tambo za kila namna zilisikika mitaani na ndani ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete ambao kwa siku tatu ulikuwa na ulinzi mkali kila kona.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo Halima Liveta amemtangaza Suleiman Mathew Ikomba kuwa amepata kura 608 dhidi ya kura 260 alizozipata aliyekuwa rais wa awamu iliyopita Leah Ulaya wakati kura moja ikiharibika.

Jumla ya wapiga kura walioripoti kwenye uchaguzi huo walikuwa 914 lakini waliopiga kura walikuwa 868.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii