Bodi ya Ligi yatoa tamko kuwa mechi ya Simba na Yanga iko palepale juni 15

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Almas Kasongo, amesema kikao cha leo kimepokea matakwa kutoka Yanga SC ikiwemo kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, na Katibu Mkuu wa TFF, pamoja na kutaka Bodi ya Ligi iwe chombo huru kisichoegemea upande wowote.

Kasongo amesema maombi hayo yamepokelewa rasmi na yatawasilishwa kwa TFF. Hata hivyo, kwa mamlaka ya Bodi ya Ligi, msimamo hadi sasa ni kwamba mchezo wa Juni 15 upo kama ulivyopangwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii