Watu 28 wafariki ajali ya gari Mbeya

Watu 28 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea usiku wa Juni 7, 2025 majira ya saa mbili usiku, katika eneo la mteremko wa Mbalizi, mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea baada ya lori la mizigo kufeli breki na kugonga magari mawili yaliyokuwa mbele yake — daladala ya abiria na kirikuu (gari dogo la mizigo). Kufuatia mgongano huo, daladala hiyo iliingia korongoni na baadaye lori hilo liliangukia juu yake, na kusababisha vifo vya abiria waliokuwemo ndani.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa majeruhi tisa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Teule ya Ifisi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii