HII HAPA ASANTE KUTOKA KWA CHETTA FLYEE

Msanii wa kizazi kipya Steven Gaudence Kinyoto maarufu kama Chetta Flyee ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la "Asante" ukiwa kama wimbo rasmi wa kwanza kwa mwaka huu 2025

Wimbo huo wenye maadhi ya bongo flavor umebeba maudhui ya kumshukuru mwenyezi Mungu " Wimbo huu ni maalumu kwa ajili ya kusema asante, nasema asante kutokana na mambo ambayo mwenyezi Mungu amenifanyia kwenye maisha yangu kwa hivyo wimbo huu ni kama sehemu ya kutoa shukrani zangu kwa aliye juu "- Chetta Flyee

Kwa upande mwingine video ya wimbo huo imetayarishwa na muongozaji wa video anaefahamika kwa jina la...... Lakini kwa upande wa audio wimbo huo umetayarishwa na mtayarishaji wa Muziki.........

Chetta Flyee ni mzaliwa wa Katavi wilaya ya Mpanda na alianza rasmi kufanya muziki mwaka 2023 ambapo pia alianzisha lebo yake inayoitwa Flyee Music Life. Mpaka hivi sasa amefanikiwa kuachia nyimbo mbalimbali sambamba na album inayoitwa " Wonders ".

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii