Polisi Wamsaka Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Apotea,

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Daniel Chonchorio, Mkazi wa Nyakato jijini Mwanza anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha majira ya asubuhi siku alipotoka kuelekea kwenye mazoezi.

Kwa mujibu wa familia ya Chonchorio wanadai aliondoka nyumbani kwake Machi 23, majira ya saa mbili asubuhi akielekea mazoezini, lakini tangu hapo hakuonekana tena wala hawakumpata kwenye simu zake za mkononi.

Ndugu wa Chonchorio wanadai kuwa tayari wametoa taarifa kituo kikuu cha Polisi Mwanza ili kujua hatima ya ndugu yao huyo.

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limethibitisha kupokea taarifa ya kupotea kwa kada huyo wa CCM na mfanyabiashara.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii