Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameondoka nchini kuelekea Vatican, kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maziko ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francisko.
Misa ya maziko ya Papa Francisko itafanyika Aprili 26,2025 mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro – Vatican na baadaye kufuatiwa na maziko yatakayofanyika katika Basilika ya Bikira Maria Majore (Santa Maria Maggiore).