Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol amea,gushwa siku ya Jumatano na upinzani na chama chake baada ya kujaribu kuweka sheria ya kijeshi siku ya Jumanne, hatua ambayo alilazimika kufuta kwa shinikizo.
Yoon Suk-yeol, ambaye kiwango chake cha umaarufu tayari kilikuwa cha chini kabisa, alitangaza kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi wakati wa hotuba ya ghafla siku ya Jumanne jioni, akishutumu upinzani kuwa ni "kikosi hasimu cha serikali" katika muktadha wa mjadala mkali wa bunge kuhusu bajeti. Lakini kutokana na uhamasishaji wa upinzani, rais ameamua kujirudi mapema asubuhi ya Jumatano, Desemba 4, na kufuta sheria hiyo aliyokuwa ametangaza.
Mkurugenzi katika ofisi ya Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol na washirika muhimu "wamewasilisha barua za kujiuzulu kwa wingi" siku ya Jumatano, kulingana na shirika la habari la setrikali la Yonhap, baada ya kuondolewa kwa sheria ya kijeshi iliyotangazwa usiku saa chache kabla na kiongozi huyo. "Washiriki muhimu wa Yoon Suk-yeol," ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa ofisi ya rais, Jeong Jin-seok, "wamewasilisha ombi lao la kujiuzulu kwa wingi," Yonhap imesema, bila kutoa maelezo zaidi. Ofisi ya rais haikujibu mara moja maombi kutoka kwa shirika la habari la AFP.
Wakati huo huo wandamanaji wamemiminika mitaani wakimtaka rais wa Korea Kusini ajiuzulu mara moja.