Vitisho vya Mabomu Vyazua Taharuki Safari za Ndege India

Ndege zisizopungua 10 za mashirika tofauti ya ndege nchini India, zimelazimika kusitisha safari zake za ndege, kuchelewesha ratiba na kubadili njia za safari zake baada ya kupokea vitisho vya mabomu ndani ya saa 48 zilizopita.

Limekuwa jambo la kawaida kwa mashirika ya ndege nchini India kupokea vitisho vya mabomu lakini kuanzia Jumatatu ya wiki hii, vitisho vimeongezeka na kuzua taharuki katika ndege hizo zinafanya safari kuelekea maeneo mbalimbali duniani.

Jumanne, Jeshi la Anga la Singapore lilituma ndege mbili za kivita kuisindikiza ndege ya Air India Express, mbali na maeneo yenye watu wengi kufuatia tishio la bomu, huku saa chache kabla ya hapo, ndege ya Air India kutoka Delhi kwenda Chicago ikilazimika kutua katika Uwanja wa Ndege wa Canada kama hatua ya tahadhari.

Awali, Jumatatu, ndege tatu za kimataifa zilizokuwa zimeondoka Mumbai, zililazimika kucheleweshwa baada ya akaunti ya X (Twitter) kuchapisha vitisho ambapo polisi wamemkamata kijana mmoja kuhusiana na tukio hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii