Fountain Gates yaja kivingine msimu wa 2024-25

Klabu ya Fountain Gates yenye makao makuu mkoani Manyara imejipanga vyema kuelekea msimu huu baada ya kukamilisha sajili za wachezaji wake wote itakaowatumia. Fountain Gate wametoa majina ya wachezaji 32 ambao kati ya hao wachezaji watano ni vijana na 27 watatumika zaidi msimu huu.

Klabu hiyo itacheza mchezo wake wa  kwanza wa ligi kuu dhidi ya Namungo huko Lindi Majaliwa Stadium  tarehe 17 na mchezo wa pili itacheza dhidi ya  Simba tarehe 25 Agosti katika dimba la KMC Complex jijini Dar es salaam. Klabu hiyo itarejea dimba lake la nyumbani la Tanzanite Kwaraa dhidi ya Ken Gold tarehe 11 September na mchezo dhidi ya Dodoma jiji tarehe 15.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii