• Jumatatu , Aprili 28 , 2025

Baerbock aunga mkono msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amesema anaunga mkono wito wa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius wa kuongezea msaada kwa Ukraine.


Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani amesema anaunga mkono wito huo pamoja na ule wa waziri wa ndani wa taifa hilo akisema kwa sasa wanachohitaji ni bajeti ya masuala ya Usalama.

Gazeti la kila Jumapili la Bild liliripoti kuwa Pistorius  anapanga kuomba msaada wa ziada wa dola bilioni 4.3 kwa usaidizi wa kijeshi wa Ukraine kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo tayari Ujerumani imetoa dola bilioni 7.1 kwa Ukraine kwa mwaka 2024.

Ripoti ya gazeti ya Bild imesema tayari pesa hizo zimeshatumika na kilichobakia ni milioni 300 ya manunuzi ya silaha nyengine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii