Mandonga Achezea Kichapo kwa Mada Maugo, apigwa TKO

Bondia Karim Mandonga amepoteza pambano dhidi ya Mada Maugo kwa kupigwa katika Raundi ya 6 kwa TKO kwenye pambano lililofanyika Mkoani Morogoro


Ngumi iliyopigwa kwenye kidevu katika pambano hilo la Raundi 6 ilimfanya Mandonga apoteze mwelekeo, ndipo mwamuzi Pendo Njau akaingilia na kumaliza pambano


Baada ya pambano, Maugo amesema “Mwalimu wangu ambaye ni mke wangu aliniambia niwe na utulivu ulingoni, hilo nimelitimiza, nikikutana na Mandonga popote pale bado nitampiga tena.”


Upande wa Mandonga amesema “Maugo hawezi kunisumbua, ni mchezo tu, uwezo wa kunipiga hana.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii