Vijana wahimizwa kufanya kazi, kutokukaa vijiweni

Vijana wanaoshinda vijiweni wakipiga soga na kucheza michezo ya bao na drafti wametakiwa kutumia muda wao kufanya kazi zitakazo waingizia kipato kwani kwani kitendo hicho kinaweza kuwashawishi kufanya uhalifu.

Hayo yamesemwa na Polisi kata ya Ruhembe Tarafa ya Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Flora Shayo alipotembelea vijiwe vya michezo ya Drafti, Bao na Pool table.

Amewaambia Vijana hao kuwa, “ni vizuri kukutana pamoja kucheza pamoja na kubadilishana mawazo lakini si sasa, muda huu nilitegemea tutakuwa shambani au kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo na hapa kijiweni tukakutana jioni.”

Mambo mengine aliyowaelimisha Vijana hao ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya Dawa za kulevya, kufichua wahalifu na kuwalinda wadogo wao wakike dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii