Bashungwa "Wakandarasi wababaishaji hapa mwiko"

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), ameagizwa kuhakikisha kuwa wakandarasi wasumbufu na wababaishaji hawapei kazi za ujenzi wa barabara nchini kote.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa alipokagua Barabara ya Handeni-Mafuleta Km 20, ambapo amesema ni aibu kuwa na mkandarasi msumbufu anaechelewesha kazi na bado kupewa miradi mingine hali inayochelewesha maendeleo kwa wananchi

“Mtendaji Mkuu nakuagiza kuhakikisha mkandarasi huyu HHEG hapewi mradi mwingine wa Km 30 mpaka nitakapojiridhisha na kasi yake ya ujenzi wa Km 20 alizonazo sasa ifikapo Januari mwakani ” amesema Bashungwa.

Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohammed Besta amesema tayari TANROADS imeshawapanga mameneja wa miradi katika miradi yote 69 inayoendelea nchini

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Handeni mjini, Ruben Kwagirwa amesema kuwa miradi mbalimbali ya barabara inayoendelea mkoani Tanga ya barabara ya Mkata -Kwamsisi (Km 36), Handeni Turiani (KM 108.2), Handeni- Kiberashi- Singida, (KM434), Kiberashi- Songe (KM 33.5) na Songe -Gairo kutaufungua vizuri Mkoa wa Tanga na kuunganisha na makao makuu ya nchi Dodoma kwa njia fupi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii