Hamilton alitaka kujiunga na Red Bull

Kwa mujibu wa kiongozi mkuu (team Principal) wa Red Bull Christian Horner amesema wawakilishi wa Lewis Hamilton walifanya mawasiliano na timu yake ya Red Bull wakiuliza kama kulikuwa na uwezekano wa Hamilton kujiunga na Red Bull kuanzia msimu wa 2024.

Christian amesema kuna watu walimtafuta na walikuwa wakiuliza kama kulikuwa na uwezekano wa Hamilton kujiunga na Red Bull watu ambao anaamini walikuwa wawakilishi wa dereva huyo rai awa Uingereza. Horner alienda mbali zaidi na kusema watu hao walifanya mazungumzo pia na mwenyekiti wa Ferrari Joh Elkann.

Sir Lewis Hamilton ambaye ni bingwa mara 7 wa Dunia amekanusha taariafa hizo akidai ya kwamba hajawahi kuwa kwenye mawasiliano ya kutaka kuamia Red Bull, isipokuwa alikuta ujumbe wa maandishi kwenye simu yake kutoka kwa Boss huyo wa Red Bull akimtaka wakutane mwishoni mwa msimu.

Inaripotiwa kuwa mchakato huu ulifanyika kabla ya Hamilton kusaini mkataba wa miaka 2 wa kuendelea kuitumikia Mercedez Benz. Hamilron Alisaini mkataba wa miaka 2 wenye thamani ya pauni million 100 zaidi ya bilioni 314 kwa fedha za kitanzania mkataba utakao muweka kwenye timu hiyo mpaka 2024.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii