Chama cha Khan chatakiwa kutafuta uongozi mpya

Tume ya uchaguzi Pakistan imekiagiza chama cha waziri mkuu wa zamani aliyeko jela, Imran Khan kiitishe uchaguzi wa kutafuta uongozi mpya ili kufanikishe ushiriki wake katika uchaguzi mkuu ujao.

Tume hiyo ya uchaguzi imetowa muda wa siku 20 kwa chama cha Tahreek el-Insaf  kufanya uchaguzi wake wa ndani ili kupata uhalali wa kuendelea kushikilia nembo ya chama chake kwenye uchaguzi huo wa mwakani. Kwa mujibu wa data za Benki ya dunia nembo au alama za vyama katika uchaguzi ni muhimu katika nchi  ambayo idadi ya watu wazima wanaojuwa kusoma na kuandika  ni asilimia isiyozidi 58. Tume imesema ikiwa chama hicho kitashindwa kufuata maagizo hayo, kitapoteza uhalali wa kushikilia nembo yake. Imran Khan amefungwa tangu mwezi  Agosti na hivi sasa anashikiliwa rumande akisubiri kusikilizwa kesi chungunzima zinazomkabili ikiwemo ya madai ya kuvujisha siri za nchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii