Kupumua ni mchakato muhimu sana ambao hauitaji
kujifunza: sote tunapumua tangu kuzaliwa na sio lazima tujizoeshe kupumua
vizuri. Je, ni kweli?
Kulingana na tafiti za hivi karibuni, inaonekana
kwamba kuna mbinu fulani ya kujifunza.
Miongoni mwa mambo mengine kwa sababu si sawa
kupumua kwa pua kama ilivyo kupumua kwa mdomo.Mtu hupumua kwa wastani kati ya
lita 10,000 hadi 12,000 za hewa kwa siku.
Hewa haijalishi ni safi kiasi gani, ina
chembechembe zilizositishwa kama vile vumbi, bakteria, virusi au vizalishaji
vya kuvu ambavyo hutua kwenye njia ya hewa na sehemu za tundu la mapafu.Lakini
tusiogope kabla ya wakati mfumo wa kupumua unajua jinsi ya kujisafisha na
kujilinda.
Ukweli ni kwamba ni chembe chembe ndogo tu
zinazoweza kufikia mapafu na kipenyo cha mikroni 3 hadi 5.Hupatikana kwa maelfu
katika utando wa ukamasi katika njia ya kupumua kila seli ya utando wa pua na
mishipa ya hewa ina silia 25 hadi 30 na urefu wa wastani wa mikroni 5 hadi 7.
Silia hujitokeza kwenye seli na kusonga kama
fagio tunapofagia. Kazi yake ni kusafisha pua yaani chembe za kipenyo cha hadi
milimita 0.5 zinazoingia zikiwavuta kuelekea kwenye koromeo ili ziondolewe
kwenye pua kwa dakika 10 au 15 tu.
Nguvu kubwa ya mashujaa hawa wa seli ni kasi yao
kuu wanatetemeka zaidi ya mara elfu moja kwa dakika wakisimamia kusukuma kamasi
inayozunguka bomba kuelekea juu na kunasa vijidudu na chembe za vijidudu kwenye
safu hii ya kamasi.
Mara baada ya hapo, mtu anaweza kuzikohoa au
zikavutwa ndani ya kinywa ambapo hakuna silia, na kumezwa. Hiyo inawafanya kuwa
utaratibu muhimu wa ulinzi dhidi ya maambukizo ya pua, matundu ya pua na mirija
ya hewa.Pua imefunikwa na mshipa wa kipekee.
Katika kiwango cha kinga pia ni maalum kwa sababu
ya vimelea vya magonjwa vinavyoingia na hewa tunayopumua.
Utando wa kamasi ndani ya pua unaendelea kuamua
kati ya kushambulia kimelea au kuruhusu kiwe, kwa sababu uharibifu
unaosababishwa na vita vinavyopigwana ndani yake itakuwa mbaya zaidi kwa mwili
wetu.
Utaratibu huu unamaanisha kwamba kuna uvumilivu
fulani kwa vimelea vya magonjwa ambavyo kwa kawaida havituletei madhara
makubwa.
Sehemu ya jukumu hilo la "ulinzi"
inatekelezwa na aina ya seli B ambayo hutoa kingamwili iitwayo IgA, tofauti kwa
kiasi fulani na IgG inayosambaa katika damu na ambayo tumesikia zaidi wakati wa
janga hili.
Kinywa kimsingi ni mlango wa chakula vigumu na
vya majimaji.
Kazi yake ni kukabiliana na vimelea vinavyojaribu
kuingia na chakula tunachokula. Kwa hiyo, kama vile tusivyokula chakula kupitia
pua, hatupaswi kupumua kupitia kinywa pia.
Kwa kuongezea, hewa inayoingia kupitia pua
hubakia joto na hufukuza vijidudu.Kupumua kwa mdomo hubadilisha mifupa ya uso
Kupumua kwa kawaida kwa kinywa kunaweza
kusababishwa na sababu za kijeni, tabia za utumiaji mbaya wa mdomo au kuziba
kwa pua, uwepo wa mianzi ya pua na kudhurika kwa utando wa pua.
Zaidi ya hayo, kupumua kupitia kinywa kunaweza
kuhusishwa na mizio ya kupumua, hali ya hewa, au kulala vibaya.Na haipaswi
kupuuzwa. Kupumua kwa mdomo kunaweza kubadilisha mpangilio wa mifupa ya uso kwa
watoto.
Kwa mujibu wa mapitio ya kisayansi kulingana na
uchambuzi wa meta, kupumua kwa njia ya kinywa husababisha mabadiliko katika
ukuaji wa mifupa ya uso na mpangilio mbaya wa meno kwa watoto kunakoweza
kusababisha mdomo kutofunga vizuri.Tatizo ni kwamba kufunga kinywa vibaya
husababisha matatizo katika kiwango cha misuli ya kutafuna, shingo, na hata
husababisha maumivu ya kichwa kwa watu wazima.
Zaidi ya nusu ya watoto wenye umri wa miaka 12
wanaugua ugonjwa wa meno kutokuwa katika sehemu yake kulingana na ripoti ya
uchunguzi wa afya ya kinywa wa 2020 iliofanywa na Jarida la Baraza Kuu la Vyuo
Vikuu vya Madaktari wa Meno Uhispania.
Kwa watu wazima, kinachostahili kufanyika ni
kurekebisha mkao ikiwa tunapumua kupitia midomo yetu: tunainamisha shingo zetu
mbele na kubadilisha msimamo wa vichwa na shingo ili kurekebisha pembe ya
koromeo na kuwezesha kuingia kwa hewa kwenye midomo yetu.Ikiwa bado
hujashawishika kuhusu faida za kupumua kupitia pua yako, jaribu kupumzika.
Utaona kwamba unapumua kupitia pua yako kwa
kawaida, wakati utahitaji kujilazimisha kupumua kupitia kinywa chako.
Tumia mdomo wako kupumua "katika dharura
tu."