GEREZA LA KUJITOLEA KOREA

Kila Nchi Inataratibu Zake Katika Kutekeleza Mambo Mbali Mbali Lakini Hili Linaweza Kuwa Moja Ya Jambo Litakalo Kuacha Na Maswali Zaidi.

Ambapo Nchini Korea Ukiachana Na Kuwa Na Magereza Mahususi Kwaajili Ya Watu Waliofanya Uhalifu Au Makosa Ya Aina Mbalimbali Pia Wameanzisha Gereza Maalumu Kwaajili Ya Kujitolea.

Bwana Ambaye Anafahamika Kwa Jina La Kwon Yung Suk Ambaye Aliwahi Kuwa Wakili Nchini Korea Ndiye Mtu Aliyegundua Dawa Ya Kushangaza Kwa Watu Wanaotafuta Njia Rahisi Ya Kuwa Na Upweke Kwa Kuwafungia Seli Kwa Siku Mbili.

 

Kwon Yung Suk Ambaye Alikuwa Mwendesha Mashtaka Wa Magereza Ambaye Alifanya Kazi Kwa Masaa 100 Kwa Wiki Kila Juma Ndani Ya Muda Wa Miezi Sita Alijikuta Akichoka Sana Kufanya Kazi Jambo Lililopelekea Kutaka Kupata Mbadala Wa Hali Hiyo.

Kwon Alimuuliza Mlinzi Mmoja Katika Moja Ya Gereza Nchini Korea  Na Mlinzi Huyo Alimwambia Kukaaa Katika Seli /Gereza Halisi Kunaweza Kumsaidia Kuondoa Hali Aliyonayo.


Inawezekana Kabisa Ni Wazo Ambalo Kwon Aliamua Kulibeba Na Unaambiwa Ilipofika Mwaka 2002 Bwana Kwon Yung Suk Alianzisha Magurudumy Ili Kuunda Mafungo Kama Jela Ambapo Watu Kama Yeye Wangeweza Kupata Amani Na Upweke.

Ilipofika Mwaka 2013 Kwon Alifungua Kituo Chake Rasmi Mashambani Kabisa Nje Ya Mji Wa Seoul Huko Nchini Korea  Kituo Ambacho Ni Gereza La Wageni Kuja Na Kukaa Siku Mbili Na Watu Hufungingiwa Kwa Masaa 20 Kwa Wakati Mmoja Bila Simu Zao,Kompyuta Mpakato Wala Saa Na Usumbufu Wowote Wa Maisha Ya Kisasa.

Licha ya kuwa watu hufungiwa katika gereza hilo kwa siku mbili hupatiwa chakula kama kawaida asubuhi,mchana na jioni,lakini pia gereza hilo lina vifaa ambavyo unaweza pia kujitengenezea chai au kahawa mwenyewe.



Pia katika gereza hilo unaambiwa kila siku kuna mazoezi mbali mbali utayafanya hasa yanayohusisha kuufanya mwili upumzike kialiki na kuwa mkimya kwa muda kadhaa Pamoja na kufanya mazoezi mbali mbali ya mwili ukiwa ndani ya chumba hicho bila kutoka .

Gereza hili utalipia pes ana kupata kifungo chako kulingana na muda unaotaka wewe kuwa katika kifungo hicho cha kujitolea.

Watu Wengi ambao hufika katika gereza hilo ni wale ambao wamechoka sana na kazi ,Pamoja na wale ambao wanapenda utulivu kiroho n ahata kuwa mbali na watu.

Je unaweza kukaa katika gereza la kujitolea.

  

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii