RAIS
wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa, (SCI), Sven Lindqueast ameitaja
Tanzania kuwa ni nchi yenye nusu ya simba wote Duniani katika Mkutano
wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii unaoendelea kufanyika nchini hapa.
Rais huyo Bw. Sven Lindquest amesema kwa hatua hiyo ameipongeza kwa juhudi za utunzaji na kupelekea wingi wa wanyama hao.
Kwa
upande wake Serikali kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro ametaja sababu zilizopelekea nchi ya Tanzania kutajwa kuwa nchi
yenye Simba wengi Duniani licha ya kuruhusu uwindaji wa kitalii.
Akizungumza
leo katika Jijini la Las Vegas nchini Marekani, Dkt.Ndumbaro amesema
nusu ya simba wote wapo Tanzania kutokana na uimara wa serikali ya
Tanzania katika shughuli za uhifadhiAmesema
kuimarika kwa shughuli za uhifadhi. hususani kwa Wanyamapori walao nyasi
ni moja ya sababu ya Tanzania kuwa na Simba wengi hivyo imepelekea
Simba nao kuongezeka kutokana na uhakika wa chakula cha kutosha .
Amefafanua
kuwa Simba hula wanyamapori walao nyasi na wanyamapori hao walao nyasi
wamekuwa wengi kutokana na uwepo wa nyasi za kutosha kutokana na
usimamizi bora wa maeneo ya Hifadhi.
"
Kubadilishwa mfumo kutoka wa kirai kwenda katika mfumo wa kijeshi kwa
Watumishi wote wanaosimamia maeneo ya Hifadhi ni moja ya sababu ya simba
kuongezeka kwa Simba nchini Tanzania" alisema Dkt.Ndumbaro.
Pia,
Dkt.Ndumbaro ameitaja sababu nyingine kuwa ni utolewaji wa elimu kwa
Jamii, amesema kwa sasa Jamii imetambua umuhimu wa wanyamapori hivyo
wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa serikali kwa kutoa taarifa
vitendo vya ujangili vinapotokea.
"
Kama nchi tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha wananchi wote wanaoishi
katika maeneo ya Hifadhi wananufaika kwa kusogezewa huduma za kijamii,
hivyo Jamii imekuwa inaona faida ya moja kwa moja ya uwepo wa
wanyamapori" alisisitiza Dkt. Ndumbaro.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amesema uwepo wa sheria kali ya
kutokuruhusu shughuli za kibinadamu kuendeshwa ndani ya maeneo ya
Hifadhi kumepelekea maeneo ya Hifadhi kubaki katika uasili wake hivyo
simba wamezidi kuongezeka kutokana uwepo mazingira salama ya wanyamapori
wengine.
Aidha,
Dkt.Damas Ndumbaro amesema licha ya Tanzania kuwa na vitalu vya
uwindaji wa kitalii zaidi ya 100 lakini imekuwa ikiendesha Uwindaji
huo kwa kuzingatia matumizi endelevu ndio maana imezidi kuongoza
Duniani kwa kuwa na simba wengi
Kufuatia
hali hiyo, Dkt. Ndumbaro amekanusha madai ya baadhi ya nchi
zinazopinga Uwindaji wa Kitalii kwa kisingizio kuwa utalii huo umekuwa
ukipunguza idadi ya wanyamapori ambapo amesisitiza kuwa Uwindaji wa
Kitalii ni muhimu kwa kuwa umekuwa ukisaidia kupunguza idadi ya
wanyamapori waliozidi ili kupunguza athari kwa binadamu.
Amesema
kwa sasa nchini Tanzania kumekuw athari kwa binadamu kutokana na
ongezeko la Wanyamapori kama vile tembo pamoja na mamba.