Papa Francis kufanyiwa upasuaji wa tumbo

Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis,  mwenye umri wa miaka 86, atafanyiwa upasuaji wa tumbo   Jumatano alasiri katika hospitali ya Gemelli ya Roma, Vatican ilisema katika taarifa.

Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, mwenye umri wa miaka 86, atafanyiwa upasuaji wa tumbo Jumatano alasiri katika hospitali ya Gemelli ya Roma, Vatican ilisema katika taarifa.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba timu yake ya matibabu imeamua katika siku za hivi karibuni kwamba upasuaji ulihitajika na kwamba anatarajiwa kukaa hospitalini kwa siku kadhaa ili kupata nafuu.

Francis alitakiwa kupelekwa hospitali baada ya mkutano wake wa kila wiki huko Vatican siku ya Jumatano asubuhi, ambapo hakutaja chochote kuhusu operesheni iliyopangwa. Alitumia dakika 40 kuchunguzwa katika hospitali ya Gemelli siku ya Jumanne.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii