Wananchi wa mkoa wa Rukwa wamepongezwa kwa kujitokeza kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa Korona ambapo hadi kufikia mwezi Januari mwaka huu watu 57,638 wamefanikiwa kupata chanjo hiyo katika vituo vya afya.
amezungumza kwenye kikao cha Umoja wa Machifu wa mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema tangu zoezi hilo la kutoa dozi za chanjo lilipoanza mwezi Julai 2021 kumekuwa na mwitikio mzuri toka kwa wananchi