CHANZO CHA KUKOROMA WAKATI WA KULALA

Kukoroma husababishwa na sauti inayotokana na mtikiso wa tishu za njia ya juu ya kupitisha hewa shughuli hii inapoendelea, hasa ikiwa njia hii ikiwa nyembamba.

Wembamba wa njia hii waweza tokana na kuziba kwa pua, uzani mzito, kuvimba kwa findo, kuvimba kwa kikoromeo au matatizo mengine, majeraha au maradhi yanayoathiri umbo la uso au shingo.

Aidha, hali hii yaweza tokea ikiwa haujalala vizuri.

Mbali na hayo, una uwezekano mkubwa wa kukoroma ikiwa wewe ni mwanamume, ukiwa mjamzito, au ukiwa mchovu.

Ili kudhibiti hali hii, usinywe pombe inapokaribia wakati wa kulala, jiepushe na matumizi ya dawa za kuchochea usingizi, dumisha uzani unaofaa, usiwe na mazoea ya kulala chali-lala kwa upande, tibiwa ikiwa una tatizo la pua kuziba, unapolala hakikisha kwamba kichwa chako kimeinuliwa.

Pia, usivute sigara, pata usingizi wa kutosha, badilisha mito yako mara kwa mara na unaweza tumia vifaa vya kuhakikisha kwamba njia ya kupitisha hewa inasalia wazi.

Mbali na hayo, unashauriwa kufanyiwa uchunguzi na mtaalamu wa masikio, pua na koo (ENT)na pia upigwe picha za eksirei ili kutambua nini hasa kibaya na upate matibabu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii