Wizi wa alama za barabarani wakithiri Shinyanga

Wizi wa alama za barabarani mkoani Shinyanga ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara umetajwa kuchangia uharibifu mkubwa wa mindombinu hiyo pamoja na kuongezeka kwa ajali za barabarani zinazochangiwa na kuibiwa kwa alama.


Wizi huo unatajwa kusababisha hasara serikali kutumia fedha nyingi kutengezeza ambapo kwa mwaka huu tayari alama 50 zimeibiwa

Licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha miundombinu ya barabara inakuwa katika kiwango kizuri, lakini bado kuna baadhi ya watu wanaiba alama za barabarani na kwenda kuuza kama vyuma chakavu hasa maeneo ya mijini huku baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakaiomba serikali kuzuia biashara ya vyuma chakavu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii