Bondia Mtanzania Stumai Muki Amchapa Chimwemwe Banda wa Malawi Dar

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Stumai Muki amefanikiwa kumchapa kwa pointi mpinzani wake kutoka Malawi, Chimwemwe Banda katika pambano lisilokuwa la ubingwa la kimataifa ililopigwa kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar

Katika pambano hilo ambalo limepigwa usiku wa Jumatano ambapo mabondia wengine wa Tanzania walioshinda mapambano ya kimataifa ni Grace Mwakamele aliyemchapa kwa pointi Luckia Ali wa Malawi wakati Zawadi kutaka naye akibonda kwa pointi Mphatso Metaudzu huku Nasra Msami akimmaliza vibaya Chiedza Homakoma kutoka Zimbabwe.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii