RAIS WA MSUMBIJI NA MKEWE WAMEKUTWA NA MAAMBUKIZI YA UVIKO 19

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mkewe Isaura wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Uviko-19.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais huyo jana Jumatatu Januari 3, 2021 imesema kuwa Rais Nyusi na mkewe wamejitenga baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

“Rais Filipe Nyusi na mkewe Isaura Nyusi wamegundulika kupata maambukizi ya Uviko-19 na wamejitenga wakifuata miangozo ya afya” imesema taarifa hiyo nakuongeza.

Hadi kufikia jana Jumatatu Msumbiji ilikuwa imerekodi kesi 193,371 za maambukizi ya ugonjwa huo, vifo 2,031 huku watu 158,680 wakiwa tayari wamepona na 457 bado wakiwa karantini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii