FAHAMU KINACHOSABABISHA NGOZI INAYOIZUNGUKA MACHO KUWA NYEUSI

Tatizo la ngozi ya sehemu inayoizunguka  macho kubadilika rangi na kuwa nyeusi huwakosesha mabinti wengi usingizi.

Hii ni shida ambayo hutokana na sababu mbalimbali kama vile uchovu, kutopata usingizi wa kutosha, kukaukiwa, anemia, mzio, kuwa wazi kwa jua, kuzeeka, uvutaji sigara, kusugua macho, maradhi ya ngozi, maradhi ya tezi au jeni.

Tatizo hili hata hivyo halipaswi kukupa wasiwasi ingawa mara nyingi tiba itategemea na vichocheo ambavyo vyaweza tibiwa kama vile maradhi ya anemia au ugonjwa wa ngozi.

Ili kukabiliana na shida hii, hakikisha kwamba unapata usingizi wa kutosha, kunywa maji kwa wingi, usivute sigara au kunywa pombe kupindukia.

Pia, kuna krimu za ngozi ambazo huenda zikatumika kurekebisha tatizo hili baada ya kupakwa kwa muda.

Lakini kabla ya kuchukua uamuzi huu, hakikisha kwamba unapata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa ngozi ili upate mawaidha kuhusu mbinu mwafaka ya kukabiliana na shida hii.

Kumbuka kuwa pia kuna mbinu za upasuaji ambazo zaweza tumika kukabiliana na shida hii.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii