HAKUNA PESA YA NYONGEZA UJENZI WA JNHPP.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP ) utakamilika bila ongezeko la gharama za ujenzi kwa sababu fedha zilizotolewa zinatosha.

‘‘Kwa dhamira na malengo ya mradi, na gharama zilizotumika, Serikali ya Tanzania haiwezi kuruhusu mradi huu kutokukamilika, kwa wenzetu wa Misri pia mradi huu ni chachu ya ushirika yenye manufaa kwao pia,‘’ amesema Waziri Makamba.

Waziri Makamba amesema kuwa timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Tanesco imepitia changamoto zilizojitokeza na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kama Rais Samia Suluhu alivyowaahidi watanzania.

Waziri wa Nyumba, Maendeleo ya Makazi na Huduma wa Misri amesema Serikali ya nchi hiyo inawahakikishia watanzania kuwa  mradi wa JNHPP utajenga uhusiano na imani kwa watanzania kuwa misri ni nchi nyenye uwezo wa kutekeleza miradi mingine mikubwa ambayo Tanzania itahitaji kushirikiana

Katika ziara hiyo Makamba aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, wa Tanzania Stephen Byabato, Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati ambao wamekagua  pia maeneo muhimu ya mradi  yanayoendelea kujengwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii