RAIS KENYATTA KUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA UHURU.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia kesho, Desemba 9 ambapo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano Desemba 8, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu amesema Rais Kenyatta atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uhuru kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa Mei 2021 alipofanya ziara nchini Kenya.

"Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa Tanzania. Amekuja mara kadhaa kikazi lakini hakuwahi kufanya ziara rasmi. Kwa hiyo, ziara hiyo itaanza kesho kwa kushiriki katika sherehe za uhuru," amesema.

Pia Akiwa hapa Nchini, Rais Kenyatta na Rais Samia watashuhudia utiaji saini Mikataba nane ya Makubaliano ambayo itahusisha masuala mbalimbali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii