Wachimbaji wa Madini watatu Wamepatikana Wakiwa Hai Siku sita Baada ya Kunaswa Shimoni.

Wachimbaji   watatu waliokuwa wamenaswa kwa siku sita shimoni Nchini Kenya  eneo la Abimbo huko Bondo, kaunti ya Siaya, wameokolewa.

Kamishna wa kaunti ya Bondo Nchini Kenya  Richard Karani alisema wachimbaji hao waliokolewa wakiwa hai na kupelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Bondo kwa matibabu, Karani alisema shughuli ya uokoaji wa mmoja wao aliyesalia shimoni inaendelea huku ikiingia siku ya saba sasa, ikielezwa kuwa ni vigumu kupitisha chakula na maji kwa wafanyakazi waliosalia walionaswa akisema wanatumia mashimo kupitisha vitu, 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii